Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Moi Voi, katika kaunti ya Taita Taveta imetangaza kusitisha kwa muda – huduma za uchunguzi wa CT scan kwa wagonjwa, kwa miezi miwili, kuanzia Machi 17 hadi Mei 7, 2026.
Katika taarifa, Msimamizi wa Hospitali hiyo Owen Juma, alisema uamuzi huo umechukuliwa “ili kuruhusu ukarabati wa kitengo cha CT scan pamoja na kufungwa kwa mashine mpya ya kisasa.”
Alisema hatua hiyo “inalenga kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wakazi wa Kaunti ya Taita Taveta na maeneo jirani.”
Ingawa kusitishwa kwa huduma hizo kutasambaratisha na kuwa usumbufu kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za CT scan, Hospitali hiyo imeeleza, uboreshaji wa huduma kama hiyo ni muhimu ili kuhakikisha huduma bora zaidi zinapatikana baada ya kukamilika kwa zoezi hilo.
Huduma za CT Scan (Computed Tomography Scan) ni uchunguzi wa kitabibu unaotumia mashine maalum ya eksirei (picha) pamoja na teknolojia ya kompyuta kuchukua picha za ndani ya mwili kwa undani zaidi kuliko eksirei ya kawaida.
Kupitia CT Scan, madaktari wanaweza kuona sehemu mbalimbali za mwili kama vile: ubongo, mapafu, moyo, mifupa, viungo vya ndani, ili kusaidia kugundua na kufuatilia magonjwa mbalimbali kama: uvimbe (tumors), majeraha ya ndani (hasa baada ya ajali), maambukizi, na matatizo ya mishipa ya damu
Ingawa kusitishwa kwa huduma hizo kutasambaratisha na kuwa usumbufu kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za CT scan, Hospitali hiyo imeeleza, uboreshaji wa huduma kama hiyo ni muhimu ili kuhakikisha huduma bora zaidi zinapatikana baada ya kukamilika kwa zoezi hilo.
Huduma za CT Scan (Computed Tomography Scan) ni uchunguzi wa kitabibu unaotumia mashine maalum ya eksirei (picha) pamoja na teknolojia ya kompyuta kuchukua picha za ndani ya mwili kwa undani zaidi kuliko eksirei ya kawaida.
Kupitia CT Scan, madaktari wanaweza kuona sehemu mbalimbali za mwili kama vile: ubongo, mapafu, moyo,
Kwa kifupi, CT Scan ni njia ya kisasa ya “kuangalia ndani ya mwili bila upasuaji,” na hutoa picha zilizo wazi na sahihi kusaidia madaktari kufanya maamuzi bora ya matibabu.
Hata hivyo, wakazi wa Voi na Taita Taveta kwa ujumla wameonekana kukerwa na hatua ya Hospitali hiyo, kusitisha huduma za CT Scan kwa miezi miwili bila kutoa suluhu mbadala kwa wagonjwa.